23 Jul 2024 / 95 views
Tetesi za soka Ulaya

Manchester United wako tayari kumuuza kiungo wa kati wa Uingereza Mason Mount, 25, msimu huu wa joto.

Kiungo wa kati wa Ufaransa Adrien Rabiot, 29, anakaribia kusaini Manchester United baada ya kuondoka Juventus mwishoni mwa kandarasi yake.

Arsenal wanajiandaa kumsajili mlinda mlango wa Uingereza Tommy Setford, 18, kutoka Ajax kabla ya ziara yao ya Marekani.

Kiungo wa kati wa Denmark Jesper Lindstrom, 24, yuko tayari kwa mkopo wa msimu mzima kwa Everton kutoka Napoli.

Brighton wamefanya mazungumzo na Inter Miami kuhusu mpango wa kumnunua kiungo wa kati wa Paraguay, Diego Gomez, 21.

Birmingham City wameelekeza macho yao kwa kiungo wa Fulham na Wales Luke Harris

Arsenal wanaongeza juhudi zao za kumsajili beki wa Italia Riccardo Calafiori, 22, kutoka Bologna.

West Ham wana makubaliano ya mdomo kumsaini kiungo wa kati wa Ufaransa N'Golo Kante, 33, kutoka Al Ittihad.

Kiungo wa kati wa Uruguay Manuel Ugarte, 23, amekubali masharti ya binafsi na Manchester United, ambao wanaendelea kufanya mazungumzo na Paris St-Germain.

Manchester United wameweka bei ya pauni milioni 30 kwa kiungo wa kati wa Scotland Scott McTominay.

Lille wanatafuta kumsajili mlinzi wa West Ham Morocco Nayef Aguerd, 28, kama mbadala wa beki Mfaransa Leny Yoro, 18, ambaye amesajiliwa na Manchester United.

Chelsea wanajiandaa kumpeleka kiungo wa kati wa Brazil Andrey Santos, 20, kwa mkopo Strasbourg tena baada ya kumalizika kwa ziara yao ya Marekani.

Everton watajaribu kumsajili kiungo wa kati wa Manchester City na Uingereza Kalvin Phillips.